23 Septemba 2025 - 16:51
Afisa wa Kizayuni anaonya juu ya kupanda kwa gharama ya kupanua vita vya Gaza

Afisa mmoja katika Baraza la Mawaziri la Israel alitahadharisha kuwa, kupanuka kwa vita dhidi ya Ukanda wa Gaza kutasababisha hasara ya ziada ya zaidi ya dola bilioni 7.5 katika uchumi wa utawala huohuo ifikapo mwishoni mwa mwaka 2025.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Afisa mmoja katika baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni wa Israel ameonya kuwa kuendelea kwa vita dhidi ya Ukanda wa Gaza hadi mwishoni mwa mwaka 2025 kutasababisha gharama za ziada za zaidi ya dola bilioni 7.5, ambayo ni zaidi ya asilimia moja ya Pato la Taifa (GDP) la utawala huo.

Hii inatokea wakati ambapo imani kwa uchumi wa Israel imeporomoka, na shinikizo juu ya bajeti ya taifa limeongezeka.

Kwa mujibu wa Bloomberg, ambaye alinukuu afisa huyo bila kutaja jina lake, gharama hizi ni zaidi ya gharama za kijeshi ambazo tayari zimefikia shekel bilioni 204 (sarafu ya Israel) katika kipindi cha karibu miaka miwili ya vita.

Afisa huyo alieleza kuwa sehemu kubwa ya gharama hizo zinatumiwa kwa:

1- Mishahara ya wanajeshi wa akiba.

2- Kununua silaha.

3- Na mifumo ya kuzuia makombora (Interceptor Systems).

Tangu kuanza kwa vita, makumi ya maelfu ya Wazayuni wameitwa kujiunga na jeshi, na kila mmoja hupokea wastani wa shekel 36,000 kwa mwezi, kiasi ambacho ni karibu asilimia 50 zaidi ya mshahara wa kawaida wa soko la ajira. Serikali huwapa malipo haya kulingana na kipato chao cha kazi ya kawaida waliyokuwa nayo kabla ya kujiunga vitani.

Bloomberg pia imeripoti kuwa athari za vita zimeenea katika maeneo mengine ya kikanda, na kusababisha gharama za kijeshi kuongezeka maradufu na kuleta mzigo mkubwa kwa uchumi wa Israel.

Gazeti hilo limeandika kuwa mipango ya utawala wa Kizayuni ya kushambulia mji wa Gaza imekumbana na upinzani mkubwa wa kimataifa, na kuna maonyo kuhusu kuzorota zaidi kwa hali ya kibinadamu na kuongezeka kwa kutengwa kwa Israel kimataifa.

Katika tathmini ya kiuchumi:

1- Wizara ya Fedha ya Israel imepunguza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa mwaka 2025 hadi asilimia 3.1.

2- Benki Kuu ya Israel nayo imepunguza makadirio yake kutoka 3.5% hadi 3.3%, kutokana na hasara za vita dhidi ya Gaza na mivutano ya kijeshi na Iran.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha